Powered By Blogger

Wednesday, June 23, 2010

KARIBUNI WADAU KATIKA BLOG HII

Bila shaka wote ni wazima wa afya njema.

Napenda kuwakaribisha katika Blog hii ambayo kimsingi imefanyiwa marekebisho kwa kuongeza au kubadili jina lililokuwapo awali. Blog hii haina tofauti sana na blog iliyoanzishwa awali iliyojulikana kwa jina la 2flag.blogspot.com. Malengo ya blog hii ni yaleyale yaliyoanzisha blog tajwa hapo juu. Hivyo nia kuu ni kuipatia blog hii jina linaloendana na maudhui au ujumbe uliomo ndani yake. Katika blog hii bado nitaendelea kutoa mchango wangu kwenye nyanja ya afya hasa inayozingatia utumiaji wa vyakula vya asili kwa afya zetu kwani ni vyakula hivyohivyo vinaweza kutumika kama dawa kwa baadhi ya magonjwa yanayosababishwa na sisi wenyewe.

Magonjwa hayo ni kama kisukari, shinikizo la damu, moyo n.k ambayo hayasababishwi na wadudu wa magonjwa isipokuwa ni kwa vyakula tunavyokula wenyewe tena kwa hiari yetu.

Kwa hiyo naomba tuungane pamoja katika kujenga afya zetu.

Asanteni na karibuni tena.